SIMBA SC ILIVYOICHAPA NKANA FC GOLI 3-1 (CAF CL - 23/12/2018)

 • Uploaded on 23 Des 2018

  Simba SC imefuzu kuingia hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) baada ya leo kuichapa Nkana FC ya Zambia magoli 3-1 katika mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Matokeo hayo yameifanya Simba ifuzu hatua hiyo kwa jumla ya mabao 4-3 kufuatia kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Zambia wiki moja iliyopita.

  Katika mchezo wa leo Nkana ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 17 kupitia kwa Walter Bwalya akimalizia kwa mpira ambao mabeki wa Simba waliuzembea kwa kufanya mchezo wa kuotea.

  Simba walitulia na kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Jonas Mkude dakika ya 29, kabla ya Meddie Kagere kupachika bao la pili kwa kichwa dakika ya 45 na baadaye dakika ya 88, Clatous Chama kuipa Simba bao la ushindi.

  Simba SC beats Zambia giants Nkana FC 3-1 in Dar Es Salaam to qualify for CAF Champions League group stage.

  Channel Azam TV

Download Links

TAGS:

Youtube Hatena . Webry . bd . Tripod . Addto . So-net . Gamer . Google+ . images . ucz . hawaii . nla . dot . bts . ed . dhs . weather