MAANDALIZI MSIMU WA KOROSHO MTWARA 2018-2019.

 • Uploaded on 19 Sep 2018

  MAANDALIZI MSIMU WA KOROSHO
  NA,OMARY HUSSEIN
  Katika maandalizi ya msimu mpya wa zao la Korosho 2018-2019 chama kikuu cha ushirika Tandahimba –Newala (TANECU) kimeanza mkakati wa kutoa mafunzo ya matuminzi ya Kompyuta wakilenga kuwafikia watendaji wote wa vyama vya msingi 123 wilayani humo lengo likiwa ni kuondoa changamoto zilizojitokeza msimu uliopita ikiwemo malalamiko ya wakulima kucheleweshewa malipo yao sambamba na kukosekana kwa kumbukumbu sahihi za malipo.
  Mafunzo hayo yanatolewa ikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa zao la Korosho, ambapo msimu uliopita changamoto zilizo jitokeza, ni pamoja na ucheleweshwaji wa malipo ya fedha za wakulima, sambamba na kukosekana kwa taarifa sahihi za malipo hayo ,hali iliyotajwa kusababishwa na kukosekana kwa vitendeakazi vya kisasa.

  Channel kuchele mtwara

Download Links

TAGS:

Youtube Hatena . Webry . bd . Tripod . Addto . So-net . Gamer . Google+ . images . ucz . hawaii . nla . dot . bts . ed . dhs . weather